Diamond, Rayvanny na Nandy washinda Tuzo Marekani


Wasanii wa Bongo Fleva,  Diamond Platnumz, Rayvanny na Nandy  usiku wa kuamkia leo Jumapili wameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA (AEAUSA) nchini Marekani.

Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA (AEAUSA) kwenye kipengele cha ‘Best Collaboration Award’ kupitia wimbo wake wa Baila.

Huku Rayvanny na Nandy kwenye vipengele vya Best Male/Female in East, South and North Africa.

Pia Mtangazaji wa kituo cha Times FM, Lil Ommy naye ameshinda tuzo ya ‘Best Host’, Huku Babu Tale akichukua tuzo ya Meneja bora wa wasanii barani Afrika.