ECG yatoa msaada kwa watoto Yatima


Na Ferdinand Shayo, Kilimanjaro

Waumini wa kanisa la ECG pamoja na viongozi wametoa misaada katika kituo cha watoto yatima cha Samaria kilichopo manisapaa ya Moshi  na kuwakabidhi mahitaji muhimu ikiwemo chakula na vifaa vya shuleni ili kusaidia kundi hilo la wahitaji.


Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 4 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo Moshi ,Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Peter Ikera amesema kuwa maadhimisho hayo yataambatana na kutembelea wahitaji na kutoa misaada ya kibinadamu pamoja na  jamii ya watu wasiojiweza.

Mkurugenzi wa kituo cha Msamaria Bw. Folkward  Mapunda amewashukuru waumini hao kwa kuwawezesha watoto hao kupata chakula cha uhakika na kuitaka jamii kuwakumbuka watoto hao.

Aidha ameitaka jamii kuiga mfano  wa kanisa hilo na kujenga utamaduni wa kuwasaidia wahitaji hususan yatima na wajane.

Watoto wanaolelewa na kituo hicho sifael john na salome wamelipongeza kanisa la ECG  kwa kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya mahitaji waliyowapatia.