Golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani, Tim Howard ametangaza kustaafu uchezaji soka baada ya kucheza mechi yake ya mwisho akiwa na klabu ya Colarado Rapids
Howard amecheza zaidi ya mechi 800 katika maisha yake ya soka. Amecheza jumla ya mechi 399 kwenye Ligi kuu ya soka England, katika klabu za Manchester United na Everton kabla ya kujiunga na Ligi Kuu ya Marekani (MLS) miaka mitatu iliyopita
Howard mwenye umri wa miaka 40 alianza kudakia timu ya taifa ya Marekani mwaka 2002, kacheza jumla ya mechi 121 timu ya Taifa, amesimama golini kwenye kombe la dunia; German 2006, South Africa 2010 na Brazil 2014.
