China yazindua setilaiti itakayotumika kwa uchunguzi wa ardhi


China imezindua setilaiti ya Gaofen-10, itakayotumika kwa uchunguzi wa ardhi, kilimo, misaada ya majanga na mikakati muhimu ya kitaifa.

Setilaiti ya Gaofen-10 ilibebwa na roketi ya masafa marefu ya March-4C, ilirushwa kutoka kwa kituo cha kuzindua setilaiti cha Taiyuan, mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa China mwendo jana asubuhi.