https://monetag.com/?ref_id=TTIb Jinsi ya kumfanya mwanamke apagawe kwako | Muungwana BLOG

Jinsi ya kumfanya mwanamke apagawe kwako

Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule.

1. Uwezo wako wa nishati
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya kukufikiria wewe mara 24/7.

2. Mbinu utakayoitumia kumsifu
Kulingana na utafiti kutoka NBC unadai ya kwamba wanawake wengi hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa kutoka kwa wanaume. Lakini usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza mwanamke inaweza kucheza pakubwa kufaulu kumpata mwanamke unayempendae baada ya muda. Afterall ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama kukuona kama wewe ni mzaha kwake.

So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo, unafaa umsifu mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu ambacho utamsifu nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza kumakinika kwa kitu ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako wa kiume kumsifia na jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa kuimba, kuchora, mtindo wake wa kutembea nk.

3. Upambo wako
Si lazima uwe mwanamume wa kuvutia ili umvutie mwanamke. Utafiti umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa mwanamume, nywele zake wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama mwanamume kuna ubaya wake mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana kama pleya ambaye unapendwa na wanawake wengi.
Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa uwe nadhifu kimwili na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu timamu halikadhalika inakufanya wewe kuwa na confidence ya kapproach demu yeyote yule.

4. Ujuzi wako wa kutangamana
Lazima atleast uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kuweza kutangamana na wengine. Kama mwanamume lazima uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kutangamana na wengine kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na ujuzi flani wa kuongea na wanawake ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya apagawe na wewe.

5. Kiwango chako cha kujiamini
Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kwako kuwa nacho ni kujiamini. Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe nayo ili uweze kuiteka hisia ya mwanamke yeyote yule

KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa yeyote yale iwapo kama hutaweza kujiamini kama mwanamume. Hivyo ni lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence. Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na mwanamke.