Kampuni ya Apple yaondoa app yake Hong Kong

Kampuni ya Marekani ya simu za mkononi ya Apple imeondoa katika simu zake app ambayo inasaidia wanaharakati wa Hong Kong kufahamu walipo polisi, kutoka katika mauzo yake ya mtandaoni leo baada ya gazeti rasmi la serikali ya China kuishutumu kampuni hiyo kusaidia tabia zilizo kinyume na sheria.

Kampuni hiyo ya Apple imekuwa kampuni ya hivi karibuni kabisa kupata shinikizo ili kuwa upande wa serikali ya China dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali, wakati gazeti la chama cha kikomunisti la Peoples Daily kusema jana kuwa app hiyo inasaidia vitendo kinyume na sheria.

Gazeti hilo liliuliza iwapo kampuni ya Apple inasaidia wahuni wa Hong Kong.

Wanaharakati wa Hong Kong wanalalamika kwamba viongozi wa Beijing na Hong Kong wanamomonyoa utawala wa mji huo na haki za raia zilizoahidiwa na mkoloni wa zamani Uingereza.