Kimbunga chasogelea maeneo zaidi Tokyo

Mvua kubwa na upepo mkali zimeshuhudiwa katika mji wa Tokyo huko Japan pamoja na maeneo ya karibu huku kimbunga Hagibis kinachotabiriwa kuwa kibaya zaidi kwa miongo sita kikipiga kusini magharibi mwa mji huo.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.7 kwenye kipimo cha Richter limepiga katika maeneo yaliyokubwa na mvua hizo, muda mfupi kabla ya kimbuga kupiga wilaya ya Shizuoka.

Tetemeko hilo lilitokea baharini karibu na pwani ya Chiba.Shirika la hali ya hewa la Japan limeonya juu ya hatari ya mvua kubwa mjini Tokyo na wilaya za karibu, ikiwa ni pamoja na Gunma, Saitama na Kanagawa.