Kituo cha msaada wa kisheria cha okoa kiwanja cha mtoto wa marehemu

Menrad Lilai, mkurugenzi wa RUPAO
Kituo cha msaada wa kisheri cha Ruangwa(RUPAO) kimeokoa  kukabidhi kiwanja cha makazi cha Ashrafu Rashid(20) ambacho alidhulumiwa na bibi yake.

Akizungumza na Muungwana Blog Mjini Ruangwa, Ashraff licha ya kukishukuru kituo hicho kwa kufanikiwa kujeshewa kiwanja hicho mikononi mwake baada ya kuchukuliwa na bibi yake( mama mzazi wa mama yake mzazi) alisema kiwanja hicho ambacho kilikuwa ni mali halali ya marehemu mama yake kilichukuliwa na bibi yake ambaye alibadili umiliki na kumpa mtoto mwingine.

Ashraff Rashid aliyezulumia kiwanja na bibi yake
Alisema alipokuwa mtoto mdogo, mama yake alifariki. Ndipo kikao cha ukoo kiliamua yeye aishi kwa bibi yake ambae alipewa jukumu lakusimamia na kutunza mali za marehemu hadi Ashraff atakapokuwa mkubwa kiasi cha kuweza kumiliki mali hizo.

''Hata hivyo bibi alianza kugawa baadhi ya vitu, hata baadhi ya nguo na vifaa vyangu alivigawa. Nilipopata umri mkubwa nilihoji hatima ya kiwanja na matofari ya mama. Nikaambiwa niende popote na nifanye chochote nitakachoweza lakini sitapata kiwanja wala tofali,'' alisema Ashraff.

Kijana huyo alibainisha kwamba kiburi na kujiamini kwa bibi yake huyo kulitokanana kubadilisha umiliki wa kiwanja hicho, ambao ulionesha mmiliki ni mtu mwingine. Hata hivyo baada ya kubanwa kwa hoja na wasaidizi wa kisheria wa RUPAO alikubali kumpa kiwanja na tofali.

Kuhusu mahusiano yake na bibi huyo baada ya kupewa kiwanja na tofali, alisema kwasasa mahusiano yameimarika na ushirikiano nimkubwa. Nibaada ya yeye na bibi yake kupewa elimu na RUPAO baada ya kusuluhishwa. Kwaupande wake mkurugenzi wa kituo hicho, Menrad Lilai alikiri kuwa katika wilaya  hiyo migogoro ya ardhi ni mingi. Nikutokana wananchi kutambua thamani ya ardhi. Hasa kutokana na ujio wa wawekezaji na ugunduzi wa madini katika wilaya hiyo.

Nae ofisa mtendaji wa kata Mbekenyera, Rajabu Rashid Mohamed alisema kituo ni msaada mkubwa kwa ofisi yake na wananchi wa kata hiyo.

Alisema wasaidizi wakisheria wamesababisha wananchi kutoa taarifa katika ofisi yake. '' Baadhi ya taarifa ilikuwa ngumu kupata, zilikuwa zinafichwa. Lakini hao waliwafichua watoto waliofichwa ndani kwasababu za ulemavu nakadhalika,'' Alisema Rajab.