Mawaziri wa Utalii na Mazingira kutoka nchi za SADC kukutana Arusha



Na Sechelela Kongola,Arusha.

Mawaziri wa Utalii na Mazingira kutoka katika nchi za Sadc wanatarajia kuwa na mkutano mkubwa utakaofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wadau wa utalii na mazingira huku jiji la Arusha likitarajia kunufaika na fursa za uwepo wa mkutano huo.

Akizungumza na Wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa mkutano huo utafanyika Octoba 18 hadi 20 mwaka huu huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo wa kimataifa ambao utajumuisha wageni zaidia 200 kutoka nchi za nje.

Mrisho Gambo amewataka Wakazi wa Arusha kuchangamkia fursa za ujio wa mkutano muhimu kufanya biashara na kuwapeleka watalii katika mbuga za wanyama na hifadhi mbalimbali zilizopo katika mkutano huo.

Aidha amesema kuwa mkoa huo uko salama hali ya ulinzi na usalama imeamarika zaidi hivyo wanawakaribisha wageni wote kufurahia mandhari ya mji huo