Michael Owen aponda kiwango cha Man United Uwanjani


Mchezaji wa zamani wa Man United, Michael Owen amesema kuwa anaamini kuwa sasa timu hiyo ni timu ya katikati (Mid-table team).

Owen akizungumza katika kituo cha BT Sport jana baada ya Man United kutoka sare ya 0-0 ugenini dhidi ya AZ Alkmaar, amesema haioni timu hiyo ikimaliza katika nafasi sita za juu katika ligi kuu nchini England msimu huu.

‘Ndio, ninaweza kusema (Man United sasa ni timu ya katikati), sifikirii watamaliza katika nafasi sita za juu, binafsi. Hii lazima iwe timu ya Man United mbaya zaidi kwa miongo kadhaasivyo?’ Owen alisema.

Mpaka sasa baada ya mechi 7 za ligi kuu nchini England msimu huu, Man United chini ya kocha wao Ole Gunnar Solskjaer wanashika nafasi ya 10 wakiwa na jumla ya pointi 9.