F Picha: Waziri Mkuu awasili Urusi kumwakilisha Rais Magufuli | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Picha: Waziri Mkuu awasili Urusi kumwakilisha Rais Magufuli

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Asha Mkuja wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Demodedovo uliopo Moscow akiwa njiani kwenda Sicho nchini Urusi kumwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya viongozi wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi. Kushoto  ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi (kushoto) na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Asha Mkuja wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Demodedovo uliopo Moscow akiwa njiani kwenda Sicho nchini Urusi kumwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya Viongozi wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa mkate na chumvi  ikiwa ni utamaduni wa kukaribisha wageni wa Warusi wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Sicho nchini humo Oktoba 21, 2019 ambako  anamwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika na Urusi