Tatizo la kutokuwepo jengo la uhakika la kuhifadhia maiti lakaribia kwisha Kilwa



Na Ahmad Mmow, Kilwa Masoko.

Tatizo la muda mrefu la ukosefu wa jengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kilwa(Kinyonga), mkoa wa Lindi linaweza kutatuliwa hivi karibuni kutokana na kasi ya ujenzi wa jengo hilo katika hospitali hiyo ya wilaya.

Hayo yamebainishwa leo mjini Kilwa Masoko na katibu wa bodi ya afya ya hospitali hiyo, Zabibu Uledi alipokuwa anasoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, ujenzi wa duka la dawa na ujenzi wa kituo cha afya cha Somanga. Kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2019, Mzee Mkongea Ali.

Uledi alisema hospitali hiyo ya Kinyonga kwamuda mrefu imekuwa na tatizo la jengo la kuhifadhia maiti. Kwani jengo lililopo ni dogo na chakavu,kwahiyo halikidhi mahitaji ya sasa yanayotokana na ongezeko la watu.

 '' Pia majokofu yake ni mabovu yanayosababisha usumbufu wakati wa kuhifadhi maiti. Kiasi cha maiti nyingine kuharibika,'' alisema Uledi.

Katibu huyo wa bodi ya afya  alisema utekelezaji wa mradi huo unaendelea vizuri. Kwani mpaka sasa jengo hilo limeezekwa na kazi ya kupiga ripu inaendelea.

Alisema ujenzi huo na waduka la kuhifadhia dawa umetumia shilingi 238,234,560 ambazo zimelipwa kwa mkandarasi hadi kufikia hatua hiyo.

Alisema wilaya ya Kilwa iliingia makubaliano  na mmoja wa wadau wakubwa wa maendeleo ya wilaya ya hiyo, kampuni ya PANAFRICAN ENERGY ambayo inajishughulisha na uchimbaji wa gesi asilia katika kisiwa cha Songosongo kwa makubaliano ya kujenga miradi mitatu ambayo ni ujenzi wa kituo cha afya Somanga kwa gharama ya shilingi 838,193,058.

'' Miradi mingine ni  ujenzi wa jengo hilo la kuhifadhia maiti ambao utagharimu shilingi 161,070,000 na duka la dawa kwa thamani ya shilingi 242,042,544. Nakufanya jumla kuu ya mradi kuwa shilingi 1,241,305,602. Nibaada ya makubaliano hayo na kampuni hiyo ambayo ilimtafuta mkandarasi anayetekeleza mradi huo baada ya kuingia nae mkataba.

Mwenge wa Uhuru upo katika siku ya kwanza kati ya mbili ambazo utakimbizwa katika wilaya ya Kilwa. Ambao hadi sasa katika wilaya hii umetembelea na kuzindua miradi mitano yenye thamani ya takribani shilingi 1.9 bilioni.