Zimbabwe: Madaktari waliogoma watakiwa kurudi kazini

Mahakama ya Kazi nchini Zimbabwe imewataka madaktari waliokuwa katika mgomo wa siku 40 wa kudai malipo warudi kazini ndani ya masaa 48, baada ya kuamuru kuwa mgomo wao ni kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo iliyotolewa jana imesema wanachama wa Chama cha Madaktari wa Hospitali ya Zimbabwe (ZHDA), wasimamishe mgomo wao mara moja.

Bodi ya Huduma ya Afya, ambayo inawaajiri madaktari hao, imesema kwamba hawakuruhusiwa kugoma kwa sababu wanatoa huduma muhimu.

Mahakama hiyo imesema ina mamlaka ya kuwachukulia hatua madaktari watakaoshidwa kutekeleza amri hiyo, na kuzitaka pande hizo mbili kutafuta suluhisho katika siku 14.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items