Thailand imefunga mbuga ya wanyama ya Khao Yai, baada ya tembo sita kuanguka na kufa wakijaribu kuokoana katika mteremko hatari wa maji wa Haew Narok.
Tembo mchanga aliteleza na kuanguka ndani ya mteremko wa maji hayo na kuvutia tembo wengine waliofika kujaribu kumsaidia.
Maafisa wa mbuga hiyo baadaye walipata mzoga wa tembo mchanga chini ya mteremko wa Haew Narok na mizoga mingine mitano karibu na hapo. Tembo wanane walianguka na kufa katika eneo hilo mwaka 1992.

