Zaidi ya Tsh. Millioni 881 za Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe zinatajwa kufanyiwa ubadhilifu ikiwemo Tsh. Milioni 400 za dawa za Hospitali na Tsh. Milioni 481 zitokanazo na makusanyo ya Halmashauri.
Akizungumzia tuhuma za ubadhilifu huo wa Tsh. Million 400 zinazowakabili watu sita akiwemo Mganga Mfawidhi wa Wilaya Revocatus Cleophace, Mkuu wa Wilaya hiyo Cornel Magembe amesema wamekuwa wakitumia password ya Mtu mwingine kufanya ubadhilifu wa dawa kutoka MSD.
Magembe amesema mbali na kuwashikilia watu hao Kamati ya Ulinzi na Usalama imetoa siku 14 kwa Mkurugenzi Mtendaji Esther Chaula, Mweka Hazina na Afisa Mapato wa Halmashauri hiyo kurudisha zaidi ya Tsh. Millioni 481 ambazo hazijulikani zilipo.
