Tutaendelea kusafirisha mafuta kwa njia yoyote - Iran

Iran imesema leo kuwa itatumia njia zozote zinaziwezekana ili kuuza nje shehena za mafuta kwa kuwa hiyo ni haki halali ya taifa hilo.

Matamshi hayo yametolewa na wazrii wa mafuta wa Iran Bijan Zanganeh ambaye amesisitiza kuwa nchi yake haitoshindwa kukabiliana na mbinyo wa Marekani kwenye sekta ya mafuta nchini humo.

 Mauzo ya mafuta ghafi ya Iran yalianguka kwa zaidi ya asilimia 80 wakati Marekani iliporejesha vikwazo dhidi ya Iran baada ya rais Donald Trump kuiondoa nchi hiyo kutoka mkataba wa nyuklia wa Iran na madola yenye nguvu mwaka uliopita.

Tangu wakati huo Washington imerejesha vikwazo kwenye mauzo ya mafuta ya Iran na nchi hiyo imejibu kwa kupunguza wajibu wake kwenye mkataba huo wa mwaka 2015 uliolenga kupunguza shughuli za nyuklia za Iran kwa ahadi ya kuondolewa vikwazo vya kimataifa.
Mpya zaidi Nzee zaidi