Vikundi vya wajasiriamali Lindi vyaungana kununua mabasi




Na Ahmad Mmow, Lindi.

Vikundi 38 vya wajasiriamali katika halmashauri ya manispaa ya Lindi vimeunganisha nguvu na kufanikiwa kununua mabasi mawili.

Hayo yameelezwa leo katika mtaa wa Mtomkavu, manispaa ya Lindi na afisa maendeleo ya jamii wa manispaa ya Lindi, Judica Sumam wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baina ya halmashauri ya wilaya ya Kilwa na manispaa ya Lindi. Sumam alisema wajasirimali hao waliamua kuungana na kununua mabasi hayo kwa ajili ya kupunguza tatizo la usafiri kwa wanafunzi wa shule za msingi na vyuo wanaoishi mbali na shule na vyuo wanavyosoma. Ambapo wazazi na walezi watachangia gharama za uendeshaji mabasi hayo ambazo ninafuu.

Alisema kwa mwaka wa fedha wa 20182019  halmashauri hiyo ilikopesha shilingi 84,000,000.00 kwa makundi mawili yenye jumla ya vikundi hivyo 38. Ambayo nipamoja na Umoja wa Wajasiriamali Lindi( UWALI) ambao unaundwa na vikundi vitatu vya mamalishe, viwili vya watu wenye ulemavu na kikundi kimoja cha vijana.

Sumam alilitaja kundi jingine la wajasiriamali hao kuwa ni Chama cha Waendesha pikipiki na Bajaj( CHAWAPIBA). Akibainisha kwamba kundi hilo linaundwa na vikundi 33 vya vijana amba
[11:42, 13/10/2019] fadi22: ao ni madereva wa pikipiki na bajaj. Hivyo kufanya jumla ya vikundi 38 vilivyo nufaika na mikopo kwa mwaka wa fedha wa 2018\2019.

Alisema halmashaur hiyo inaendelea kutekeleza maelekezo ya serikali ya kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuyawezesha kiuchumi makundi hayo maalumu.'' Kwakufanya halmashauri inatekeleza kwa vitendo sheria ya bajeti namba kumi na moja ya mwaka 2015, pamoja na sheria ya fedha ya Serikali za Mitaa sura ya 290 kifungu cha 37A(4) pamoja na kanuni zake za mwaka 2019 zinazohusu utoaji na usimamizi wa mikopo kwa makundi hayo,'' alisema Sumam.

Miongoni mwa faida mikopo kwa makundi hayo ni kuwapa mitaji  inayowazesha kuongeza vipato kwa ajili ya kusomesha watoto wao, kuwawezesha kujenga nyumba bora, kuwajengea misingi ya kukopesheka katika taasisi za fedha na kuandaa mazingira wezeshi ya kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.