Vipimo visivyo rasmi sasa basi


Adelina kapaya, Katavi

 Meneja wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Katavi, Phanuel Matiko amepiga marufuku matumizi ya Vipimo visivyo rasmi Maarufu kama vikale au ndoo kwa Wafanyabiashara wa mazao ya chakula na biashara kwani nikinyume cha sheria ya vipimo Tanzania

Hayo yamebainishwa na Matiko ambapo amewataka wafanyabiashara kutumia vipimo vinavyotambulika kisheria ili kuepuka usumbufu kwani ni kinyume cha sheria kutumia vipimo ambavyo havijapigwa chapa na kukaguliwa na wakala wa vipimo.

Sheria ya Vipimo Tanzania sura ya 340 kifungu cha 35-41 kinamtaka wakala kufanya ukaguzi na kupiga chapa mzani ili kuhakikisha vipimo vinavyotakiwa kutumika viko sawa kulingana na mujibu wa sheria unavyomuongoza .

Matiko amesema atakaebainika anatumia vipimo visivyo rasmi atashtakiwa na kutozwa faini isiyo chini ya laki moja na isiyopungua laki tano kwani atakua amekiuka sheria ya vipimo Tanzania .

Licha ya hayo sheria inamtaka mmiliki wa mzani ahakikishe kila anapotimiza mwaka mmoja anatakiwa kupeleka mzani wake kwa wakala wa vipimo ili kuuhakikiwa  na kupiga chapa kwani mzani unavyozidi kutumika ndivyo unavyozidi kupoteza ubora

Matiko amesema wamekua wakitoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya matumizi ya vipimo ambavyo vinatamburika kisheria licha ya wengi wao kutotumia vipimo vinavyotakiwa  na pia ametoa ushauri kwa wafanyabiashara ambao hawatoweza kumudu gharama ya kununua Mzani  waungane kundi ili wachangie pesa kwa ajili ya kununua Mzani kwani inaweza kuwa njia rahisi ya kununua Mzani.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa huo wamesema kuwa licha ya tamko hilo kutolewa bado kunachangamoto ya wafanyabiashara kuwa na mitaji midogo ambayo haitosherezi kununua mzani hivyo inawalazimu kutumia vipimo visivyo rasmi

Kutokana na sheria ya Vipimo inayomtaka Wakala kuhakikisha Vipimo vinavyotumiwa na wafanyabiashara havipingani na vipimo vinavyotamburika kisheria  Menaja Wakala wa Mkoa wa Katavi amelazimika kupiga marufuku matumizi ya Vipimo hivyo licha ya baadhi ya wafanyabiashara kutoridhika na maamuzi hayo.