Na. Timothy Itembe, Mara
Mfumo Dume kikwazo cha kufikia malengo ya 50-50 wanawake kujitokeza kuwania uongozi katika nyadhifa mbalimbali wilaya Tarime mkoani Mara Chama cha mapinduzi kimebainisha.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Khamisi Mukaruka jana wakati akiongea na Mwandishi wa habari Ofisini kwake jinsi walivyojipanga kuwainua wanawake kuwania uongozi kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikiali za mitaa 2019,11,24 alibainisha kuwa mfumo dume ni kikwazo kwa Mwanamke kugombea.
Mukaruka alisema kuwa mikakati waliyonayo ni kuona wanawake wanajitokeza kwa wingi kuwania nyadhifa katika nafasi zinazogombewa lakini kikwazo ndani ya jamii ya kabila la kurya kuwaruhusu wanawake kugombea ni mfumo dume.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa hivi majuzi ndani ya Kijiji cha Gibaso kulitokea tukio la kulaani kuelekea kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wafuasi wa vyama vya siasa kwa maana ya Chadema na CCM kuchaniana Bendera hali Bendera hazina makosa tukio ni la kulaani kwani linaashiria uvunjifu wa Amani na ni kikwazo kwa wapiga kura.
“Ndani ya wilaya Tarime kuna matawi ya chama cha Mapinduzi 116 kwa maana ya Tarime Mjini matawi 28 huku Tarime vijijini tukiwa na matawi 89 pia mabalozi tulio nao ni 1447 kwa maana ya Tarime vijijini mabalozi 232 na Tarime Mjini mabalozi 32 kwa hali hiyo kipaumbele cha wagombea nafasi nyingi bila ubaguzi tumeacha furusa hiyo wanawake kugombea lakini mfumo dume inaonekana umewaadhiri ambapo hadi sasa waliojitokeza kwa idadi niwachache kuliko wanawake nasikia tetesi”alisema Mukaruka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Demokorasia na Maendeleo CHADEMA wilaya Tarime,Mwita Joseph alisema kuwa kwa mjibu wa Ibara ya 8 ya katiba yetu inasema Mwananchi ndio msingi na Mamlaka juu ya Serikali iliyopo madarakani.
Joseph alitumia nafasi hiyo kulaani kitendo cha baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa kujiingiza katika vitendo vya kiuhalifu ikiwemo kuchana Bendera za vyama huku hazina makosa na kudai kuwa hivyo ni moja ya viasharia vya uvunjifu wa Amani.
Kiongozi huo alibainisha kuwa kuna haja kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Tarime kuchukua jukumu la kuwakalisha pamoja viongozi wa vyama vya siasa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa ili kuzungumzia mstakabali wa Amani.
Joseph alitaja kuwa kuna baadhi ya viongozi ndani ya vyama vya siasa wanatumia nafasi waliyonayo ama wanatumia mabavu na madaraka yao waliyo nayo kuwatisha wananachi na hata kuwatumia vijana kuvuruga Amani jambo ambalo halikubaliki kikatiba.
Kuhusu Chama chake kuwapa nafasi ya kugombea wanawake ndani ya Chama alisema kuwa wao wanazingatia katiba na katiba inaruhusu kwa hilo hawana wasiwasia nalo atakaye jitokeza watamsimamisha kugombea.
Naye Winfrida Clement- mkazi wa mtaa wa Bugosi ameahidi kugombea nafasi ya mwenyekiti wa mtaa huo kupitia Chama cha mapinduzi na kumung'oa mwenyekiti wa Chadema aliyepo Zacharia Ghati.
Awali mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikaliTGNPlinalojishugulisha na kupinga ukatili wa kijinsia,Lilian Liundi alisema kuwa mapambano dhidi ya ukatili wa kinsia ni kuhakikisha kuwa mila kandamizi zinazomnyima mwanamke nafasi ya kugombea zinaachwa nyuma na hazipewi nafasi.
