Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye wamememlilia Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (Tiss), Apson Mwang’onda (75) aliyefariki dunia jana nchini Afrika Kusini.
Taarifa za familia yake zinaeleza kuwa Mwang’onda alikuwa akisumbuliwa na saratani alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na baadaye kuhamishiwa nchini humo.
Bashe ameandika "Nimepokea kwa masikitiko na uchungu , taarifa za kifo cha baba yetu, rafiki, mshauri, kiongozi na mzee wetu mpendwa Colonel Apson Mwang’onda, mtu ambaye wakati wote wa safari yangu ya kisiasa na uongozi alikuwa msaada mkubwa usiomithilika. Pumzika kwa amani baba."
Nape ameandika "Simba amefunga macho! Nchi imepoteza kichwa chenye uwezo wa kipekee! Familia imepoteza muhimili muhimu! Mimi nimepoteza mentor and a friend! A man with great heart! Pumzika Baba."
