Wasichana wapania kuwania uongozi


Na. Rahel Nyabali, Tabora

Baadhi ya wasichana mkoani Tabora wamesema hawata kuwa nyuma kuwania nafasi za uongozi  katika chaguzi  za Serikali  za mitaa  na uchaguzi mkuu  ujao wakiamini kwamba kupata uongozi  kutawasiadia  kuimarisha  nguvu  katika  kukabiliana  na vitendo  vya  ukatili  wa  kijinsia  vinavyodaiwa  kuua  ndoto za  maisha yao.


Wameyasema hayo wakati  wakizungumza kwenye kongamano la Ajenda ya msichana ya  2019  lililoandaliwa  na  Shirika  lisilo  la kiserikali  la  Msichana Initiative  lililofanyika  Chuo  cha  utumishi  wa  umma  ambapo  zaidi ya  wasichana  elfu  kutoka  wilaya  ya  Nzega,Uyui  na Tabora  mjini  walishiriki.

Akifungua kongamano hilo mkuu wa mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri amesema Serikali  itaendelea  kukabiliana  na vitendo  vya  ukatili wa  kijinsia  ambavyo  kimsingi  vinadaiwa  kuwaathiri Wasichana kimwili  na  kisaikolojia na hivyo kusababisha  kuwazorotesha  kifikila na kiuchumi   kiuchumi ikiwemo kuwania uongozi .

Aisha uledi ni moja ya msichana walio huzulia kwenye amesema semina hiyo imewasaidia kwa kiasi kikubwa kwa wasichana  kujitambua na kuweza kuwania kuwania nafasi za uongozi.

Mkurugenzi mtendaji Msichana Initiative Rebeca Ryumi amesema hii itaweza kusaidia jamii kuona ni jinsi  gani  msichana  anaweza  kuonesha  na  kutumia  nguvu  zake  kama  chachu  ya maerndeleo na  kukomesha   ukatili  wa  kijinsia.

Aidha Mkoa wa Tabora ni  miongoni mwa  mikoa mitatu  nchini  inayoongoza  kwa  vitendo  vya  ukatili  wa  kijinsia  ambapo  Shirika  la  Msichana Initiative  linatekeleza  mpango  wa  kuwajengea  uwezo  wasichana  ili  iwe kichocheo  kushiriki  vita  dhidi  ya  vitendo  vya  ukatili  wa  kijinsia  hususani  mimba  na  ndoa  za  utotoni.
Mpya zaidi Nzee zaidi