Wizara ya madini yafuta Leseni 156 za wachimbaji wa madini Kagera



Na Clavery Christian Kagera.

Waziri wa madini Dotto Biteko amesema kuwa wizara yake tiali imefuta leseni 156 za wachimbaji wa dhahabu mkoani Kagera ambao hawaonekani ili hizo leseni waweze kupewa wachimbaji wadogo ili agizo la mh, Rais Magufuli liweze kutimia la kuwapa maeneo wachimbaji wadogo.

Hayo yamesemwa na waziri wa madini Dotto Biteko leo mjini Bukoba mkoani Kagera wakati wa kukabidhiwa jengo la kituo cha umahili mkoa Kagera na SUMA JKT baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo.

Amesema kuwa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani alitaka sekta ya madini ibadilike ihame kwenye uchimbaji wa kubabaisha na ujanjaujanja iwe sekta ya wachimbaji na wadau wa uhakika na wanaofuata sheria ambapo amesema kuwa ili wachimbaji waweze kuwa wachimbaji wa uhakika na wenye kufata sheria lazima mazingira fulani yaandaliwe ya kuwafanya wawe kwenye huo urasimu ambapo amesema kuwa Rais Magufuli tayali ameishaielekeza wizara kutoa maeneo ya kuchimba kwa wachimbaji wadogo.


Waziri Biteko ameupongeza uongozi wa mkoa Kagera kwa kusimamia shughuli za maendeleo zinazotekelezwa mkoani humo kikamilifu bila ya kuwepo mapungufu yeyote katika miradi hiyo.

"Sababu kubwa ni kwamba wajenzi wenyewe walikuwa kwenye mazingira rafiki Nivigumu sana kuwaibia wanajeshi wakiwa wanajenga lakini kuna mahala wanaibiwa lakini kwenye mkoa Kagera hatujasikia malalamiko yeyote ya watu wa Kagera wakija kuiba au kufanya uharibifu wa miundo mbinu ambayo imejengwa na haya yote yamewezekana kwasababu upo uongozi makini ambao upo chini yako mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya mwenyeji na kamati zenu za ulinzi na usalama ya mkoa na ya wilaya, ni imani yetu kama wizara ya madini kwa miradi ambayo tutakuwa tunaipata ya kupeleka mikoani Kagera itakuwa sehemu moja wapo kwasababu tunauhakika vitu vyote viko salama vikiwa kwenye mkoa Kagera" Amesema Dotto Biteko waziri wa madini.

Aidha waziri Biteko amempongeza mkandarasi wa mradi huo ambaye ni SUMA JKT kwa uaminifu wake na utendaji kazi bora na kumaliza kwa wakati ujenzi wa miradi wanayokabidhiwa na waizara ya madini akitolea mfano ujenzi wa ukuta wa merelani mkoani Manyara akisema kuwa SUMA JKT waliiondolea hofu serikali waliyokuwa wanapewa na wakandaradi wengine wakati wa kuomba mikataba.

Jengo la umahili la madini mkoani Kagera limegharimu tsh, bilioni 1.08 za kitanzania jengo ambalo litatumika katika shughuli mbalimbali zinahusu madini.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items