Rais Magufuli azindua miradi miwili akiwa ziarani mkoani Songwe



Na Baraka Messa, Songwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ameanza ziara yake ya siku mbili mkoani Songwe kwa kutembelea miradi miwili ya uzinduzi wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha GDM kilichopo mji mdogo wa Mlowo na kuweka jiwe la Msingi mradi wa upanuzi wa huduma ya maji katika mji wa vwawa

Akiongea na wananchi baada ya kukagua miradi ya maji na kiwanda cha kahawa katika mji wa Vwawa alisema mkoa wa Songwe pamoja na kuwa mkoa mpya ni miongoni mwa mikoa ambayo inafanya vizuri katika sekta ya maendeleo ukilinganisha na mikoa mingi mikongwe, huku akimpongeza Gervas  Mwangoka kwa kufugua kiwanda ambacho kinatengeneza ajira kwa vijana wengi na kulipa kodi kwa Serikal.

‘’nimefurahishwa sana na miradi hii miwili niliyoitembelea kwa sababu ni miradi mizuri tena ya mifano ndio maana nmeongeza milioni 100 kwenye mradi wa maji ili kuongeza mashine za kusukuma maji ili lita zitoke milioni tatu kama alivyosema wazir wa Maji toka lita zaidi ya milioni moja ambazo zinatoka hivi sasa, pia kwewnye ule mradi wa kiwanda nimeagiza patengenezewe kiwango cha rami kwenda kiwanda cha kahawa hii ni kutokana na kijana huyu mzalendo alivyofanya kazi nzuri ya uje wa kiwanda bora kabisa” alisema Rais Magufuli.

Alisema mkoa wa Songwe unakumbwa na changamoto nyingi kutokana na upya wake lakini unafanya vizuri katika Nyanja mbalimbali hasa kilimo na maendeleo kwa ujumla .

“mkoa huu ulianza rasmi Januar, 29 mwaka 2016 lakini ni mkoa ambao unakua kwa kasi sana ukilinganisha na mikoa mingi mikongwe hapa nchini , mkoa mpya ulishika nafasi ya tatu kwa uzalishaji ukitanguliwa na mikoa ya Rukwa na Ruvuma , kwa nini tusiujengee soko la kisasa la mazao na stendi nzuri ya mkoa” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameupongoza uongozi wa Mkoa wa Songwe ukiongozwa na mkuu wa mkoa Brigedia Jeneral Nicodemas Mwangela kwa kukamilisha ujenzi wa ofisi ya mkoa wa Songwe na kubakisha bilioni mbili kati ya bilioni sita (6) ambazo zilitengwa kwa ajili ya kukamilisha ofisi hiyo ya mkoa.

Alisema mkoa wa Songwe viongozi wake wanastahili pongezi kwa uzalendo waliouonyesha katika usimamizi wa miradi ya maendeleo na kusababisha mkoa kwenda kasi licha ya kuwa mkoa mchanga.

“hela mlizo zitumia vizuri na kubaki siwezi kuzichukua zikaenda sehemu nyingine , mmesema mnamaboma mengi ambayo mmeyajenga hivyo naomba hizo bilioni mbili zipelekeni huko zikaboreshe na kukamilisha miundo mbinu katika shule zote za mkoa wa Songwe ili kuwapunguzia michango wanchi wa Songwe” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Nicodemas Mwangela awali akitoa salamu za mkoa alisema kuwa mkoa ulitengewa shilingi bilioni sita (6) kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mkoa lakini kutokana na usimamizi mzuri wapo mwishoni kukamilisha jengo hilo huku wakiwa wamenunua vifaa vyote kwa ghalama ya bilioni nne na kubakisha bilioni mbili (2) ambazo alimuomba rais kuzibakisha Songwe ili zitumike kukamilisha maboma ya madarasa.

Pia Mwangela alimwomba Rais kujenga kituo cha mafunzo ya kilimo na ufugaji ili kuongeza uzalishaji na kuwajenga vijana wanaomaliza shule waweze kujiajili kutokana na hivi sasa mkoa huo kukosa vyuo vya ufundi kuanzia ngazi ya mkoa mpaka wilaya wakati vijana wengi humaliza shule.

Kesho (leo) Rais wa Jamhuri nya Muungano wa Tanzania ataendelea na ziara wilayani Momba kwa kutembelea miradi ya ujenzi hospitali ya mji wa Tunduma Mpemba kwa kukagua na kuweka jiwe la Msingi , kuweka jiwe la Msingi utengenezaji barabara ya Mpemba –Isongole Ileje na kuzindua mradi wa huduma za pamoja mpakani Nakonde na Tunduma akishirikiana na Rais wa Zambia Edgar Lungu.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items