Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelitoa wito wa kubadilisha mifumo ya chakula ili hali ya janga la njaa na uharibifu wa chakula iweze kupungua.
Alitoa ombi hilo katika ujumbe wa video wa Siku ya Chakula Ulimwenguni ambayo husherehekewa kila ifikapo Oktoba 16.
Siku ya Chakula Ulimwenguni ni wito wa kupunguza janga la njaa ulimwenguni, katika ulimwengu ambapo chakula kizuri kinapatikana na cha bei rahisi kwa kila mtu, kila mahali. Lakini leo, zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosha.
"Haikubaliki kwamba janga la njaa linaendelea kuongezeka wakati ulimwengu unapoteza zaidi ya tani bilioni 1 za chakula kila mwaka." alisema Antonio Guterres.
