Tsh. Milioni 110 kujenga matundu ya vyoo 100 Mtwara


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa kiasi cha Tsh. Milioni 110 kuchangia kampeni ya 'Shule ni Choo Msitiri Mwanafunzi na Mwalimu' iliyozinduliwa leo mkoani Mtwara.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema fedha hizo zitatumika kujenga matundu ya vyoo 100 katika mkoa huo.