Vikosi vya uokozi vilitumia matrekta kuwatafuta watu walio hai ambao wamenasa kwenye ghorofa za juu za majengo leo baada ya tetemeko kubwa kuikumba Albania majira ya asubuhi na kusababisha vifo vya watu 14 na wengine 600 wamejeruhiwa.
Tetemeko hilo lililokuwa katika kipimo cha 6.4 lilifika katika eneo lote la kusini mwa Balkan na kufuatiwa na matetemeko mengine madogo madogo.
Katika nchi jirani ya Bosnia, tetemeko lingine likiwa katika kipimo cha 5.4 lililikumba eneo la kusini mashariki ya mji mkuu na pia lilifika hadi Sarajevo. hakuna ripoti za haraka za watu waliofariki na ni uharibifu mdogo tu uliotokea.
Tetemeko nchini Albania lilivunja karibu majumba matatu wakati watu wamelala, na vikosi vya uokozi vilikuwa vinafanyakazi kuwapata watu ambao wanaaminika kuwa wamenaswa katika vifusi vya majengo hayo.
Hakuna taarifa za watu wangapi huenda bado wamefunikwa katika vifusi hivyo. Wizara ya afya imeripoti kuwa kiasi watu 600 wamejeruhiwa, baadhi wakiwa katika hali mbaya.