Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema limewaondoa wafanyakazi wake 49 kutoka Beni, mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, usiku huku kukiwa na ongezeko la hali ya kutokuwa na usalama, katika mapambano dhidi ya Ebola.
Shirika hilo la afya la Umoja wa Mataifa limesema limepeleka zaidi ya theluthi ya wafanyakazi wake 120 mjini Beni na Goma, kwenda kusini zaidi katika mpaka wa mashariki wa nchi hiyo, kutokana na ongezeko la hali ya kutokuwa na usalama.
Lakini limesema wafanyakazi muhimu 71 wataendelea kubakia katika mji huo kuendelea na kazi ya kudhibiti kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola ambapo watu 2,200 wamefariki.
Hali ya kutokuwa na usalama imetatiza zaidi juhudi za kuzuwia Ebola tangu kuzuka kwa ugonjwa huo hivi karibuni katika jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuanza Agosti mwaka 2018.
Lakini ghasia katika eneo hilo la mashariki ambalo halina utulivu, zimeongezeka , ambapo raia 77 wameuwawa katika mji wa Beni tangu Novemba 5, kwa mujibu wa shirika lisilokuwa la kiserikali kundi la utafiti la Congo, (CRG.).