AliKiba ajibu kuachana na Meneja wake


Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka kuachana na Meneja wake, Seven Mosha aliyekuwa akifanya nae kazi.

Alikiba alisema kuwa hajaachana na Meneja wake huyo, isipokuwa wamegawana majukumu na ndio maana watu kwasasa wanamuona amechangamka tofauti na mwanzo.

"Sijaachana na Seven, ila tumegawana majukumu kwasababu kuna Business zinatufanya tudelay katika upande mwingine wa muziki kwasababu hata mm mwenyewe nilikuwa taiti kweli kweli safari, mikutano siunajua eeh nasafiri sana," alisema Alikiba katika mahojiano yake na Clouds FM.

"Wakati mwingine watu hawajui niko wapi lakini tumeona tuongeze watu tufanye nao kazi kama unavyoona tumehangamka tofauti na ilivyokuwa awali kwahiyo wasishangae."
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items