Watafiti wasio na vyeti hawana nafasi kufanya tafiti - DC Kasesela


Watafiti wote wanaofanya utafiti Tanzania wametakiwa kufanya utafiti wakiwa na elimu ya utafiti kutoka chuo cha takwimu hapa nchini au nje ya nchini kwa lengo la kuondoa takwimu zisizo sahihi ambazo zimekuwa zikileta migogoro kwenye jamii.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wadadishi wa utafiti wa mwaka 2019 kwa niaba ya
mkuu wa mkoa wa Iringa, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema kuwa watakwimu wote wanatakiwa kufanya tafiti wakiwa na cheti kinachomsibitisha kuwa ni mtakwimu.

"Wanaojiita mtakwimu yeyeto yule lazima awe na cheti ambacho kinamdhibitisha kuwa ni mtakwimu na amesaini maadili ya takwimu la sivyo atakuchuliwa hatua za kisheria na pia hataruhusia kufanya kazi za kitafiti katika eneo usiku," alisema Kasesela.

Kasesela alisema kuwa watakwimu wakitoa takwimu ambazo sio sahihi sinaleta tatizo kwenye
usalama wa taifa kwa unakuwa umetikisa usalama wa taifa.

“Huyu mama na watu wake ni muhimu sana kwa usalama wa nchini kwa kuwa wanatoa takwimu
zilifanyiwa kazi na zimethibitishwa na mamlaka husika” alisema Kasesela

Aidha Kasesela amesema kuwa watafiti wengi wanatakiwa kurudi darasani ili kuwasaidia kutoa takwimu zilizo sahihi na zisizoleta madhara kwa usama wa taifa.

Awali akitoa maelezo kwa ufupi kwa mgeni rasmi,mtakimwi mkuu wa serikali Dr Albina
Chuwa amesema kuwa watatumia technolojia ya hali ya juu kukusanya takwimu zilizo sahihi kwa muda mfupi.

“Utafiti huu kwa weledi wa juu wa kutumia teknolojia ya Kisasa ya kusanya takwimu Nchi
nzima kwa muda mfupi na kupunguza gharama na Utafiti huu umgefanyika miaka kumi kumi iliyopita ungegharamiwa kwa Tshs. Bilioni 5 lakini kwa matumizi ya teknojia ya Tablets imepunguza gharama kwa nusu,Utafiti huu utagharimu TShs. Bilioni 2 na Matokeo yatatolewa mwezi Desemba 2019,” alisema Chuwa.

Hata hivyo Chuwa alisema dhahiri teknolojia kwa kiasi kikubwa imepunguza gharama za kufanya
Tafiti hapa Nchini na nitumie nafasi kutoa wito kwa Watakwimu wote Nchini kuwa ni vyema tujikite zaidi katika kuendeleza kujifunza zaidi teknolojia za kisasa za kuchakata taarifa za Kitakwimu kwa kuwa kwa sasa Dunia kila siku mbinu mpya za kitakwimu zinaendelea kufanyiwa majaribio na kutumika na Maofisi ya Takwimu Duniani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items