Loading...

11/30/2019

Baada ya kumchapa Tinampay, Hassan Mwakinyo amtaka Manny Pacquiao na Amir Khan


Baada ya bondia Hassan Mwakinyo usiku wa jana kumchapa Arnel Tinampay wa ufilipino kwa pointi, ametangaza kutamani kuwaona Manny Pacquiao na Amir Khan wanatua bongo kuzichapa.

Akiongea na Azam TV, baada ya kumalizika kwa pambano hilo, Mwakinyo alisema anatamani Manny Pacquiao na Amir Khan waje Tanzania acheze nao maana haamini kama kuna utofauti wa ngumi.

"Huu ni mwanzo tu, tunamtaka Manny Pacquiao na Amir Khan waje Tanzania hapa tucheze nao. Mimi siamini kama kunautofauti wa ngumi, ngumi nilizocheza mimi ndio alizocheza Mfilipino ingawa mimi nipo Tanga na yeye yupo Ufilipino kwa Manny Pacquiao," amesema Mwakinyo.
Pia Mwakinyo amefunguka sababu ya kutofanya vizuri kwenye pambano lake la jana dhidi ya Tinampay huku akitaja sababu kubwa iliyomuangusha ni gloves alizovaa sio zile ambazo amezoea kupigana nazo. 
"Niliamini kwenye ufiti wangu hajakutana na mtu anayeweza kupiga. Nimegundua kitu kinachombeba siyo bondia mkali bali ni mvumilivu sana. Hata mimi sijaridhika ila kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, kama unaona kabla ya pambano kulikuwa na maongezi ya muda mrefu sana kwa sababu walikuwa wanasema gloves nilizovaa hazifai. Nimevaa gloves ambazo sijazizoea sijawahi kucheza nazo pambano lolote ni mara ya kwanza," amesema.

Mwakinyo ameongeza, "Siyo kama sijacheza vizuri ila nimeridhika kutokana na mchezo jinsi ulivyokuwa unaenda, kwa sababu ningekuwa kwenye form yangu ile ninayoitaka mimi ningekuwa huru kucheza na gloves ambazo nimezoea kucheza nazo."

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger