Chama cha soka cha England FA kimemfungia mechi moja na kumpiga faini ya Pauni 50,000 (Tsh Mil 148) nyota wa Man City Bernardo Silva kwa ku-post kitu kilichotafsiriwa cha kibaguzi kwa mchezaji mwenzake Benjamani Mendy.
Mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, Silva aliposti katika akaunti yake ya Twita picha ya Benjamin Mendy akimfananisha na katuni iliyopo katika Chokoleti ziitwazo Conguitos za nchini Hispania.

