Benki za Zimbabwe zimeanza kutoa Noti na Sarafu mpya zilizotolewa na Benki Kuu ya nchi hiyo (RBZ) ili kupunguza ukosefu wa sasa wa Pesa Taslim
Watu walitarajia kuanza kupata pesa hizo kuanzia Jumatatu kutokana na tangazo la awali la Benki Kuu, lakini noti hizo hazikupatikana kutokana na Benki kutumia siku hiyo yote kukusanya pesa mpya kutoka Benki Kuu
Hata hivyo, baadhi ya wateja wamelalamika kuwa kiwango cha chini cha kuchukua pesa katika Benki ni Dola 50 kwa wiki, ingawa kiwango cha juu zaidi cha kuchukua pesa ni Dola 300
Mhudumu mmoja wa Benki ya biashara amesema, wanatarajia kuongeza kiwango cha kuchukua pesa endapo wataendelea kupata pesa za kutosha kutoka Benki Kuu
