Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa swali la Kambi ya Upinzani leo halijaulizwa kwa Waziri Mkuu kwasababu kiongozi wa kambi hiyo Freeman Mbowe ni mtoro.
Spika ametoa kauli hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu maarufu kama maswali ya 'PAPO KWA PAPO'
"Kabla hatujaendelea Waheshimiwa Wabunge naomba niwakumbushe tu kuwa utaratibu wetu kipindi chetu cha Maswali kwa Waziri Mkuu swali la kwanza kabisa huwa linakuwa ni la Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni na ndio utaratibu wetu," amesema Spika Ndugai.
"Kwahiyo hatujapata swali lile kwasababu kiongozi huyo hayupo na kama hujaja Bungeni na Spika hana taarifa zako wewe ni mtoro. Ndiyo maana mara nyingi mnaona fursa hii inapotea potea hivi sababu ya utoro."
