Waziri Mkuu akiri kuwepo kwa uhaba wa Chakula


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekiri kuwepo kwa uhaba wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini, aeleza sababu na mikakati ya kukabiliana na uhaba huo.

Leo Bungeni jijini Dododoma akijibu swali la Mbunge Juma Nkamia aliyesema kuwa baadhi ya mikoa ina kabiliwa na tatizo kubwa la chakula huku akisema kuwa yawezekana viongozi hawatoi taarifa kwa kuwa na uoga kutokana kutoelewa vizuri Agizo la Rais.

"Upungufu wa Chakula upo kwa baadhi ya Wilaya na maeneo kadhaa na huu ulitokana na tatizo la hali ya hewa kwamba yapo maeneo msimu uliopita hatukupata mvua za kutosha," amesema Waziri Mkuu.

"Jambo hili linapotokea kule kwenye ngazi hiyo tunao viongozi na tumeweka utaratibu kama serikali wa viongozi walio kwenye maeneo hayo kuratibu shughuli zote ikiwemo na haya ya kutokana na hali ya hewa."