Boris Johnson asema wafungwa wa ugaidi hawapaswi kutolewa jela mapema

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema watu waliotiwa hatiani kwa makosa ya ugaidi hawapaswi kuruhusiwa kutoka jela mapema, baada ya kubainika mtu aliyewashambulia watu kwa kisu mjini London hapo jana alitolewa jela mwaka mmoja kabla ya kifungo chake kumalizika.

 Mshambuliaji huyo Usman Khan aliyewahi kufungwa jela kwa miaka sita kutokana na makosa ya ugaidi aliwauwa watu wawili na kujeruhi wengine watatu karibu na daraja mashahuri la mjini London.

Mkuu wa polisi ya kupambana na ugaidi mjini London, Neil Basu, amesema mwanaume huyo alikuwa akihudhuria mafunzo ya kuwaelimisha wafungwa wakati alipofanya shambulio hilo.

Waziri Mkuu Johnson amesema mwenendo wa kuruhusu wahalifu katili kutolewa jela mapema umeonesha kutofanya kazi nchini Uingereza.

Wakati huo huo Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza ametuma salamu za rambirambi kufuatia mkasa wa mjini London alioutaja kuwa wa kikatili.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items