Mamia waandamana kudai haki ya waliouwawa Sudan

Mamia ya waandamanaji wamemiminika katika mitaa ya mji wa Khartoum leo, kudai haki kwa ajili ya watu waliouawa kwenye maandamano dhidi ya rais aliyeondolewa madarakani Omar al-Bashir.

Waandamanaji wakusanyika katikati ya mji mkuu, Khartoum na kuelekea ofisi ya waziri mkuu Abdalla Hamdok, wakizitaka mamlaka kutoa haki kwa watu waliopoteza maisha na kuwatafuta waandamanaji ambao bado hawajulikani walipo.

Kulingana na muungano harakati za uhuru na mabadiliko, zaidi ya watu 250 waliuawawa na mamia kujeruhiwa wakati wa maandamano ya miezi kadhaa, ambayo yalizuka mwezi Desemba mwaka jana.

 Bashir aliyeitawala Sudan kwa mkono wa chuma kwa kipindi cha miaka 30, aliondolewa na jeshi katika mapinduzi ya Aprili 11 baada ya maandamano yaliyochochewa na mgogoro wa kiuchumi.