F Godbless Lema achaguliwa kuwa mwenyekiti CHADEMA kanda ya kaskazini | Muungwana BLOG

Godbless Lema achaguliwa kuwa mwenyekiti CHADEMA kanda ya kaskazini


Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini katika uchaguzi uliofanyika leo Jumamosi Novemba 30, 2019 mjini Arusha

Katika uchaguzi huo Lema alipata kura 78 na kumshinda mpinzani wake mbunge wa Rombo, Joseph Selasini aliyepata kura 27.

Wakati akijinadi Lema alieleza kuwa anawania nafasi hiyo kukitumikia chama hicho na kujiandaa kuwa mwenyekiti wa Taifa

Katika uchaguzi huo  mbunge wa Viti Maalumu, Yosepher Komba alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kanda hiyo kwa kupata kura 76 kati ya 106

Kwa upande wake Selasini amesema atashirikiana na Lema kuhakikisha mikoa ya Kaskazini inaendelea kuwa ngome ya Chadema