Loading...

11/10/2019

BREAKING: Rais Magufuli afanya uteuzi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi 4 za Taasisi za Serikali na Mkuu wa Chuo mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Alexander Lugatona Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

3. Mhe.Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board).

4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Felician Bakamaza Kilahama kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).

Wenyeviti hawa wa bodi wameteuliwa kushika nyadhifa hizo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, na uteuzi wao umeanza tarehe 09 Novemba, 2019.

5. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Shadrack S. Mwakalila kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Memorial
Academy).

Prof. Mwakalila anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili na uteuzi wakeumeanza tarehe 08 Novemba, 2019.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger