Burkina Faso yaipa onyo kali Ufaransa

Ofisi ya mkuu wa majeshi wa Burkina Faso imeionya  Ufaransa kuhusiana na nchi hiyo kurusha ndege zake katika anga la nchi hiyo bila kutoa taarifa kwa serikali, onyo hilo limesisitiza kwamba ndege yeyote itakayoruka katika anga la nchi hiyo bila ruhusa itachukuliwa kama shambulizi la adui na watakachofanya ni kuitungua.

Mkuu wa majeshi, Moise Miningou aliarifu kwamba Ufaransa imekuwa ikitumia anga la nchi hiyo bila ruhusa kurusha ndege zisizo na rubani na ndege nyingine za kawaida.Alivitaka vitendo hivyo vikomeshwe mara moja kwani baada ya onyo hilo watavichukulia vitendo hivyo kama shambulizi la adui na hivyo kuzitungua.