Dk Shein amesema SMZ inaendelea kuimarisha miundombinu ya Usafirishaji



Na Thabit Madai, Zanzibar.

Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na jitihada mbali mbali za kuimarisha miundombinu ya Usafirishaji Nchini

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa Uzinduzi wa Boti KILIMANJARO VII katika viwanja vya Hotel ya Verde Maruhubi Mjini Zanzibar.


Dk. Shein amesema Lengo la serikali ni kuleta Maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo ya Usafiri inayotegemewa na Wananchi.

Alisema  Sekta ya Usafiri inachangia kwa kiasi kikubwa Maendeleo ya Nchi pamoja na kuimarisha miradi ya Wawekezaji katika huduma za Maendeleo ikiwemo Utalii,Biashara na Kilimo.

Dk Shein aliwataka Wawekezaji kutumia fursa zilizopo Zanzibar katika kuwekeza Miradi ya Maendeleo katika sekta mbalimbali ili kuimarisha ukuwaji wa Uchumi Nchini.

Aidha Dk Shein alisema  ni vyema kwa Wawekezaji kuekeza Vitu vyenye ubora hususan Vyakula na Vyombo vya Usafiri ili kuepuka athar zinazoweza kujitokeza hususan kwa watumiaji wa Usafiri wa Baharini pamoja na kwenda sambamba na Utejelezaji wa Sera ya Nchi katika usafiri.

Akitowa Maelezo ya boti hiyo kwa Naiaba ya Mmiliki wa Mradi, Abuubakar Azizi Salim amesema Kampuni ya Bakharesa itaendelea kuwekeza katika usafiri wa Bahari ili kuungamkono juhudi za serikali juu ya kuimarisha huduma ya Usafiri kwa wananchi.

Alisema  licha ya Kampuni hiyo kuwekeza katika sekta ya usafiri lakini wamekabiliwa na tatizo la kukosa nafasi ya kutosha katika eneo la abiria katika Bandari ya Malindi jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa kwa abiria wakati wa kupanda boti na kushuka.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk.Muhammed Ramia  amesema Serikali itahakikisha inazifanyia kazi sera na sheria za Wawekezaji ili kuwawezesha Wawekezaji kuwekeza bila ya vikwazo.

Boti hiyo ya KILIMANJARO VII imetumia miezi 18 kutengezwa hadi kukamilika ambapo ina tabaka 4 za kukaa abiria na unauwezo wa kuchukuwa abiria 510.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items