Faru weupe kupandikizwa hifadhi ya Burigi Chato kwa mara ya kwanza Tanzania



Na Clavery Christian Biharamulo Kagera.

Waziri wa maliasili na utalii dr. Khamisi Kigwangala amesema kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania ipo katika mikakati ya kupandikiza Faru weupe katika hifadhi mpya ya Burigi Chato baada ya kuona ukubwa wa hifadhi na mandhari yake vinafaa kwa wanyama hao.

"Tumeamua kupandikiza Faru weupe kwa mara ya kwanza Tanzania bado utafiti unaendelea namna watakavyoweza kuishi katika hifadhi hii hawakuwai kuwepo kabisa lakini tumeona mandhari yake, ukubwa wa hifadhi lakini pia utamaduni wa faru weupe kwamba wanazaliana sana na kwa haraka sana watatusaidia sana katika nchi hii kuongeza idadi ya Faru na katika kuwaifadhi kwa faida ya dunia nzima" Amesema Waziri Kigwangala.


Mh, Kigwangala amesema hayo katika ziara yake ndani ya hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato na wasanii mbalimbali ikiwa ni ziara ya kuhamasisha watanzania kuja na kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi za taifa za Burigi Chato pamoja na wanyama mbalimbali wanaopatikana humo.

Mh, Kigwanagala amesema kuwa Faru weupe ni wazuri katika kutunza watoto tofauti na Faru weusi huku akisema kuwa sababu zilizopelekea Faru weusi kupungua na kufikia hatua ya kutoweka kabisa ni kwasababu Faru weusi siyo wazuri kulea na kutunza watoto kama Faru weupe.

"Sababu inayopelekea kuwa na Faru weusi ni kwamaba walikaribia kutoweka kabisa kwahivyo tumeanza jitihada za kuwarejesha lakini Faru weusi hawatunzi vizuri sana watoto wao kwahivyo watoto wanaliwa sana na fisi na wanyama wengine mbalimbali kwa sababu anawaacha watoto mbali yaani Faru mweusi siyo mama mzuri wa kulea watoto lakini Faru mweupe wanakaa sana katika familia na kutunza watoto na kwahivyo watoto wanawaweka watoto katikati na watoto wanakuwa salama tofauti na Faru weusi na hivyo tukileta Faru weupe tutakuwa na uhakika ndani ya kipindi kifupi kupata Faru wengi hapa nchini" Amesema Kigwangala.


Waziri wa maliasili na utalii mh, dr Khamisi Kingwangala ametembelea maeneo mbali mbali na wasanii mbalimbali wa Tanzania na kujionea wanyama wengi wanaopatikana katika hifadhi ya taifa Burigi Chato.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items