Hatuwafukuzi wakimbizi - Lugola


Serikali ya Tanzania imekanusha tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba imekua ikiwafukuza wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika Makambi na Makazi  mbalimbali mkoani Kigoma,Tabora na Katavi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola baada ya Mkutano wa kutiliana saini kati ya pande tatu ikiwemo Serikali ya Tanzania, Serikali ya Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) lengo ikiwa ni kuwarudisha wakimbizi walioomba kurejea nchini Burundi kwa hiyari yao  baada ya amani kurejea nchini humo

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani  kutoka nchini Burundi Pascal Barandagiye amesema nchi ya Burundi kwa sasa kuna amani na wanaomba raia wao warejee ili waweze kuijenga nchi yao.

Nae Kamishna Msaidizi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR ,George Okoti Obbo amesema wameshirikiana na nchi mbili za Tanzania na Burundi katika kufikia makubaliano hayo wakiamini Tanzania imekua nchi inayopokea raia wanaopata matatizo katika nchi zao na akiwashukuru raia wa Tanzania kwa ukarimu wao.