Iran imeanza rasmi kururutubisha upya madini ya urani katika kituo cha Fordo. Habari hizo zimetangazwa na shirika la n guvu za atomiki la Iran.
Hapo awali Rais Hassan Rohani alizungumzia kuhusu "awamu ya nne" ya hatua za kujitoa katika makubaliano ya kimataifa kuhusu mradi wa kunklea wa Iran na kusababisha hofu ulimwenguni.
Shughuli za kurutubisha madini ya urani katika kituo hicho cha chini ya ardhi cha Fordo zilisitishwa kutokana na makubaliano ya kimataifa ya mradi wa nuklea wa Iran yaliyofikiwa mwaka 2015.
Rais Donald Trump wa Marekani ameitoa nchi yake mwaka 2018 katika makubaliano hayo.