Mchezaji Kinda wa Atletico Madrid na timu ya Taifa ya Ureno Joao Felix ameshinda tuzo ya Golden Boy 2019 baada ya kuwapiku Makinda wengine 18 wakiwemo Jadon Sancho (England & Borussia Dortmund) na Kai Havertz (Ujerumani & Bayer Leverkusen) ambao walikuwa wakimfuata kwa ukaribu.