Katibu mkuu wa UN amsifu Merkel kuhusu mazingira

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameisifu sera ya serikali ya Ujerumani kuhusu mazingira kuwa kama mfano wakati wa mkutano na kansela Angela Merkel mjini Berlin.

Guterres amesema anaishukuru Ujerumani kwa kuchukua jukumu la mbele la kuongoza hatua za mabadiliko ya tabia nchi ikiwa kama mfano wa uwajibikaji duniani na maadili ya jumla.

Akizungumzia kuhusu mpango wa mazingira wa Ujerumani, ambao umeanzishwa na serikali ya sasa ya muungano, Guterres amesema, huu ni mchango mkubwa katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Katibu mkuu amesema kuwa ana matumaini nchi nyingine zitafuata mfano uliowekwa na Ujerumani.

Hatua za mabadiliko ya tabia nchi , ambazo ni pamoja na bei ya utoaji wa gesi za kaboni katika sekta ya usafiri na ujenzi, hata hivyo imekumbana na ukosoaji kutoka kwa walinzi wa mazingira, ambao wanasema hauendi mbali vya kutosha.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items