Kamati za Dini mbalimbali mkoa wa Manyara zajipanga Kukomesha Ukatili



Na John Walter-Manyara

Ukatili wanaofanyiwa wakina mama na Watoto katika baadhi ya maeneo hapa nchini umezifanya dini mbalimbali kuungana kwa pamoja ili kuweza kuisaidia jamii kuondoka na ukatili huo.

Kongamano hilo lililofanyika mjini Babati limeratibiwa na Shirika la Kimataifa la Norwegian Church Aid  (NCA).


Wakizungumza katika Kongamano maalum la Viongozi  wa dini mbalimbali mkoani Manyara  zinazoundwa na Baraza kuu la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA),Wamesema lengo lao  kuu  ni utekelezaji wa Malengo endelevu  ifikapo mwaka 2030  katika Kutokomeza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi vinavyoweza kuzuilika,Kutokomeza ukosekanaji wa taarifa na huduma  za afya ya uzazi kadri ya imani za dini na kutokomeza ukatili wa kijinsia na mila potofu zinazochochea matendo ya kikatili.

Mchungaji Niiteeli Panga wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKT) Babati amesema  ni muhimu taasisi za kidini na serikali kufanya kazi kwa kushirikiana kwa mujibu wa miongozo ya dini kuhusu njia zinazofaa kiumri katika kuelimisha vijana juu ya masuala ya afya ya uzazi na kutomeza ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Sheikh wa mkoa wa Manyara Muhammad Kadidi amesema dhamira ya imani za wakristo na waislamu ni amani upendo na msaada kwa wahitaji na kukuza uelewa kwa jamii zetu na kutetea haki ya jinsia kwa wote.

Akitoa ushuhuda Lucy Manda mkazi wa Dareda amesema ameshuhudia vitendo vingi vya kikatili vikitokea lakini  baadhi ya wazazi wamekuwa wakipokea Rushwa ili kumaliza kesi Kinyumbani.

Kaimu mkurugenzi wa idara ya Afya na ustawi wa jamii (BAKWATA.)  amesema Takwimu za mwaka 2015-16 zinaonyesha mkoa wa Manyara ulikua na vifo 376 kati ya vizazi laki moja  ambapo vifo hivyo vimeshuka na kufikia  68 kati  ya vizazi laki moja kwa mwaka 2018.

Mmoja wa mwanachi Lucy Manda aliyeshiriki mkutano huo  akatoa ushuhuda wa jinsi watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na baadhi ya wazazi kuyamaliza mambo hayo nyumbani katika eneo la Dareda analoishi huku akiitaka jamii kuacha tabia hiyo ili kulinda haki za watoto.