Katibu wa CCM Longido aagiza watu hawa kukamatwa


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Longido, Laigwanani  Ezekiel Mollel amewaagiza Maafisa Tarafa wa Wilaya hiyo kuwakamata Viongozi wanaofanya vikao visivyo rasmi vya kuwakwamisha Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji waliochaguliwa kwani uchaguzi umeisha  hivyo wanapaswa kushirikiana  na walioshinda kuleta maendeleo.

Akizungumza na wenyeviti wa  vijiji 48 na wenyeviti wa vitongoji 176 katika hafla fupi ya kuwaapisha amewataka Viongozi waliochaguliwa kuvunja makundi na kuondokana na vikao vya kuwajadili viongozi waliochaguliwa.

Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya longido, Natanagwak Mollel amesema kuwa baadhi ya viongozi wamekua wakitumia vibaya fedha za wananchi kujinufaisha badala ya kupeleka sehemu iliyokusudiwa hivyo kuzua malalamiko na kusababisha migogoro isiyo ya lazima hivyo iwapo watabainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items