Waziri mkuu wa Kuwait amewasilisha barua ya kujiuzulu hii leo sambamba na baraza lake la mawaziri. Hatua hiyo inafuatia madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya mawaziri na ukosoaji juu ya utendaji kazi wao.
Waziri mkuu Sheikh Jaber Mubarak Al-Sabah, aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Kadhi mkuu, ili kuruhusu mabadiliko ya mawaziri.
Waziri wa fedha wa nchi hiyo alijiuzulu mwezi uliiopita kuepuka kuhojiwa bungeni, kwa madai ya kukiuka sheria ya Kiislamu kwa kutoza riba katika mikopo iliyochukuliwa na wastaafu kutoka shirika la pensheni la taifa.
Waziri mwingine wa kazi naye alitangaza kuachia ngazi baada ya kubanwa bungeni juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kadhi mkuu endapo atakubali barua ya kujiuzulu anaweza kumteua tena waziri mkuu huyo au kumteua mtu mwingine kuunda serikali mpya.
Kuwait ni taifa pekee katika nchi za Ghuba kuwa na bunge kamili lililochaguliwa.