Maafisa 53 wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wameshiriki kikao cha Bunge leo asubuhi kwa lengo la kutangaza kampeni ya Utatu inayoshiriki TAKUKURU.
Akizungumza Bungeni Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Andrew Chenge ameipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri wanayoifanya nchi nzima.
