Waziri Mkuu awataka Wafanyabishara kuchangamkia fursa ya kusambaza chakula


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wafanyabiashara nchini kuchangamkia fursa ya kusambaza vyakula kwenye maeneo ambayo hayana chakula ili kujikwamua kiuchumi.

Ametoa wito huo Bungeni leo, katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata chakula kwenye maeneo yenye uhaba.

"Nitoe wito kwa wafanyabiashara wetu nchini, Tanzania maeneo yote haya yana hali ya hewa tofauti yako ambayo yalipata mvua nyingi na walizalisha chakula cha kutosha na yapo ambayo hayakuwa na mvua za kutosha na hakuna chakula cha kutosha hivyo ni jukumu la wafanyabishara wetu kutumia fursa hiyo kwa kuhamisha chakula kutoka maeneo yenye chakula cha kutosha na kupeleka kwenye maeneo ambayo hakuna ili waweze kujipatia uchumi,” amesema Majaliwa.

Aidha amesema kuwa bado kuna umuhimu wa mkuu wa wilaya kuiandikia wizara ya kilimo kueleza mazingira hayo na kwa utaratibu wa wizara ya kilimo wanaweza kwenda kwenye maeneo hayo kujionea na kujiridhisha takwimu iliyotolewa halafu waruhusu chombo chao kupeleka mahindi kwa kuuza ili wananchi wapate fursa ya kununua.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items